Mjumbe wa nyumba kumi katika eneo la Kinondoni Jijini Dar es salaam, Rashidi Mashaushi jana aliamka na bahati ya pekee baada ya kujikuta akizungumza na Rais John Magufuli ambaye alimpatia kiasi cha sh. 200,000 alipowasilisha kero ya mafuriko mtaani kwake.

Akizungumza na Dar24 Media mtaani kwake Mashaushi amemshukuru Rais Magufuli kwa kumpatia kiasi hicho cha fedha.

Amesema kuwa amefarijika sana alivyoweza kuwasilisha kero ya mafuriko kwa rais Magufuli ambayo imekuwa ikiwasumbua kwa muda mrefu.

“Kwakweli jana ilikuwa kama nimeokota dodo kwani sikutarajia kupata kiasi hicho cha fedha, hivyo Mungu ambariki sana azidi kuwa na moyo wa kuwasaidia wanyonge,”amesema Mashaushi

 

Huu ndio ukweli kuhusu jumbe za uhamasishaji
Hizi hapa sababu 7 za kutumia limao kila siku asubuhi