Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema kuwa atahakikisha anafanikisha ujenzi wa Ofisi za kisasa 402 za walimu pamoja na Vyoo kwa shule za Msingi na Sekondari zilizobainika kuwa na upungufu wa huduma hizo.

Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa Ofisi hizo za kisasa zitakuwa na sehemu ya Chumba cha Mwalimu Mkuu,Chumba cha Muhasibu, Chumba cha Katibu Muktasi pamoja na ofisi za Msaidizi wa Mwalimu Mkuu na walimu wote huku zikiwa na Vyoo vya kisasa pamoja na Bafu.

“Siwezi kuwa na amani kama walimu wangu hawana ofisi wala vyoo katika shule 402, ni aibu na fedhea kwa walimu kugombania choo na wanafunzi au kutumia vyoo vya majirani au Bar, hii sio heshima ya mwalimu wa Mkoa wangu, ndio maana nimeamua kuanza kufanyia kazi changamoto hizi,” Amesema Makonda.

Aidha, Kutokana na gharama za ujenzi kuwa kubwa Makonda ameviomba vyombo vya Ulinzi na usalama vya Mkoa wa Dar es Salaam kumpatia mafundi wa ujenzi kama sehemu ya kuunga mkono jitiada alizoanzisha za ujenzi wa Ofisi hizo ambapo vyombo hivyo vimeridhia kumuunga mkono.

 

Hata hivyo, ameongeza kuwa ataanza kutembelea viwanda vinavyojihusisha na uzalishaji wa vifaa vya ujenzi ikiwemoMabati, Saruji, Nondo na vinginevyo kuona namna wanavyoweza kuunga mkono ujenzi huo ili kuhakikisha walimu wanafanya katika mazingira rafiki

Magazeti ya Tanzania leo Agosti 2, 2017
Video: Sumaye afunguka mazito kuhusu Wema Sepetu