Mjumbe wa nyumba kumi kutoka Kinondoni Jijini Dar es salaam, Rashid Mashaushi amesema kuwa anayo mengi ya kumueleza rais Dkt. Magufuli.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Dar24 Media ambapo amesema kuwa kama angeweza kupatiwa muda zaidi angeweza kumueleza kero nyingi zaidi.

“Kwanza namshukuru sana rais wetu msikivu kwa kutusikiliza sisi masikini na wanyonge, kama ningeweza kupewa muda zaidi ningeweza kumueleza kero nyingi ambazo hazijui zinatukabili sisi wanyonge,”amesema Mzee Mashaushi

 

TCRA yataka watumia Facebook, Instagram, Twitter kujisajili
Hamisa, Diamond bega kwa bega wafuturisha yatima