Rais wa Marekani, Barack Obama amemkaribisha Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump Ikulu (White House) leo ili kuanza kujadili kipindi cha Mpito na kukabidhiana madaraka kama ilivyo utamaduni wa demokrasia ya Marekani.

Rais Obama ametoa wito kwa Wamerekani kuungana pamoja, pia ameagiza timu yake kufuata mfano wa timu ya Rais George W. Bush miaka minne iliyopita na kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha kipindi cha Mpito cha Rais Mteule kinafanikiwa kwani wote wanamtakia ufanisi katika kuwaunganisha pamoja na kuiongoza Marekani.

Video: Watu katika miji saba Marekani waandamana kumpinga Trump
Twiga Stars Kuwapima Wenyeji Wa Fainali Za Afrika 2016