Rais wa Marekani,  Barack Obama amemuidhinisha rasmi Hillary Clinton kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Democratic akimwagia sifa za kuwa na vigezo kuliko yeyote aliyewahi kugombea.

Obama ametangaza uamuzi wake huo kupitia kipande cha video cha dakika tatu ambapo amesema kuwa anafahamu kazi ya urais wa taifa hilo na hajawahi kuona mtu ambaye ana vigezo vingi zaidi ya Hillary Clinton katika nafasi hiyo.

“Sidhani kama kumewahi kuwa na mtu aliyehitimu kuishika hii nafasi [zaidi ya Hillary Clinton],” alisema Obama.

“Nataka wote waliokuwa name tangu mwanzo wa safari hii nzuri kufahamu kuwa wa kwanza kufahamu kuwa ‘niko naye’. Nimelipuka. Niwezi kungoja kufika kule na kuanza kufanya kamepni na Hillary,” alisema Obama.

Kabla ya kutoka kwa video hiyo, Obama alikutana na mshindani wa Hillary Clinton katika chama chake Bernie Sanders na kufanya naye mazungumzo.

Sanders ameahidi kumuunga mkono Hillary Clinton ili waweze kupambana na kumshinda mgombea wa Republican, Donald Trump.

Video: Mayweather amsifu Justin Bieber kwa kupigana na Shabiki aliyemzidia
Mbunge wa Chadema akana elimu inayomtambulisha Bungeni