Rais wa Marekani Barack Obama ametoa hotuba yake ya mwisho kama Rais wa Marekani ambapo amewahimiza Wamarekani kuitetea demokrasia.

Obama ametoa hotuba hiyo jana mjini Chicago, maelfu ya watu waliokusanyika kumsikiliza walionekana kujawa na furaha na hisia kubwa, ambapo Obama amewaeleza kuwa kwa kila kipimo, Marekani sasa ni bora zaidi, na ina nguvu zaidi kuliko ilivyokuwa miaka minane iliyopita alipochukua madaraka.

Amesema hata hivyo demokrasia inatishiwa kila inapokosa kutiliwa maanani.

Hivyo, Obama amewaomba Wamarekani wa kila asili kusikiliza wengine wanasema nini huku wakitazama misimamo ya wengine, “lazima tuwategee sikio wengine na kusikia” – Obama.

 

Rais Barack Obama ndiye Rais wa kwanza nchini Marekani wa asili ya Afrika, alichaguliwa mwaka 2008 ambapo aliahidi kurejesha matumaini na kuleta mabadiliko.

Donald Trump ambaye ndiyo mrithi wake ameahidi kubatilisha baadhi ya sera kuu alizofanikisha Rais Obama.

Schneiderlin Kuondoka Old Trafford Saa 48 Zijazo
Lowassa asikitishwa na Ukawa