Bosi wa PKP, Ommy Dimpoz ambaye aliwahi kukwaruzwa na mashairi tata ya rapa Nay wa Mitego, amkejeli rapa huyo kwa majanga aliyoyapata ya kushushiwa rungu na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA).

Ommy ambaye ameeleza kuwa hana tatizo lolote na rapa huyo hata kama alimuimba vibaya kwani anajua ndio aina ya muziki anaofanya, amesema hivi sasa rapa huyo amejitengenezea shida kwani aina ya muziki aliouzoe umezuiwa.

Uzuri kama sasa hivi Tanzania, BASATA imeshaanza kudeal na wanamuziki wasiojielewa…. Sasa hivi inabidi akiandika awapelekee kwanza BASATA waangalie, sasa ni shida amejitengenezea mwenyewe,” Ommy Dimpoz aliiambia The Playlist ya 100.5 Times Fm.

“Na Nay asipoimba vile anavyotaka kuimba, ngoma yake ni ngumu. Kwasababu hawezi kutuimbia vitu vya maana tukamuelewa, tumeshamzoea… tukana tukuelewe, na BASATA haitaki matusi, basi tafuta biashara [nyingine],”aliongeza.

Nay alikumbwa na majanga ya kufungiwa nyimbo zake kadhaa ikiwemo ‘Pale Kati’.

Hivi karibuni, Ommy aliachia video na audio ya wimbo wake mpya aliomshirikisha Ali Kiba, wimbo uliobatizwa jina la ‘Kajiandae’.

Yahya Hamad Kaimu Mwenyekiti Kamati Ya Saa 72 Ya TFF
Faustino Asprilla: Cristiano Ronaldo Ni Mbinafsi