Tamasha la magari Tanzania (Autofest) linatarajiwa kufanyika Oktoba 28 hadi 30, 2016 katika viwanja vya Biafra, Kinondoni jijini Dar es salaam, ambapo litakuwa ni onyesho la magari mapya na matoleo mapya ya pikipiki likihusisha matukio ya ‘Cone Challenge’, ‘Sprint Zone’ na ‘Drifts’ likiwa na kauli mbiu isemayo ‘Kuendesha tunaelekea wiki ya usalama barabarani’.

Akiongea na waandishi wa habari mapema leo Oktoba 26, 2016, Mkurugenzi Mtendaji wa Vision Investment, Ally Nchahaga amesema kuwa tamasha hilo litakuwa kubwa sana kwani litaonyesha magari ya abiria, magari ya biashara, piki piki, bodi za magari sehemu za magari, mashine na zana zinazohusiana na magari.

Amesema watu wengi wanashindwa kutunza magari yao inavyopaswa kutokana na elimu ndogo, hivyo lengo lao ni kuleta aina mbali mbali ya bidhaa ya vyombo vya moto na huduma kwenye ‘Autofest’ ili wadau wapate kujifunza na kufurahia bidhaa. Amesema mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage

Aidha, Mkurugenzi huyo mesema onyesho hilo linategemea kuvutia zaidi kwani mwaka huu wameongeza kuchangia damu kushirikiana na Damu Salama, ili kuwasaidia wahanga wa ajali wanaotaabika juu ya uhitaji wa damu kutokana na upungufu katika akiba ya damu.

Video: Jeshi la Polisi Dar lawashikilia wachina kwa utekaji, lakusanya Sh. mil. 6.9 kwa siku 7
Manuel Neuer: Schweinsteiger Anaweza Kutoa Msaada