Msanii wa muziki wa dansi nchini, Johnson Nguza maarufu kama Papii Kocha kwa mara ya kwanza baada ya kutoka jela ameachia wimbo  wake mpya unaoenda kwa jina la ”Waambie” uliobeba mashairi yenye hisia kali yanayoiaminisha dunia uwepo wa Mungu katika maisha ya kila siku na kuwakumbusha walimwengu kuwa palipo giza nene ndio nyota ina mwanga mkali.

Papii kocha ambaye alifungwa kwa zaidi ya miaka 13 jela na kutoka kwa msamaha wa Rais John Pombe Magufuli siku ya maadhimisho ya Miaka 56 ya Uhuru amekuwa akifanya kazi hizo za kimuziki mpaka pale mahakama ilipomuhukumu.

Ujio wake mpya ni dallili nzuri kwani amefanya wimbo wenye mashairi mazuri yanayojenga hisia kali na imani kali juu ya kumwamini Mungu, ni shuhuda tosha ya maisha ya msanii huyo juu ya mapito aliyopitia.

”Mungu waambie ni wewe tu, uliyesababisha leo imefika ” ni moja ya mstari katika mashairi ya wimbo huo.

Katika wimbo huo ameimba kuwa binadamu hawapaswi kukataa tamaa sababu daima Mungu hayupo mbali.

Amesema ”wasiache tumaini ndio imani, wasiache kukuamini mtoa imani”

Wimbo huo umeandikwa na mwanadada Natasha na kutengenezwa na mtayarishaji wa muziki wa bongo fleva Ema The Boy na video yake kutengenezwa na Wanene Studio.

Itazame zaidi hapa.

Majaliwa atoa agizo kwa Halmashauri zote nchini
Video: JPM amuapisha Dkt. Slaa kuwa balozi