Nyota wa klabu ya Real Madrid na Timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo amefungua hoteli ya aina yake yenye muonekano wa uwanja wa mpira katika mji wa Madeira nchini Ureno.

Hoteli hiyo yenye jina, Pestana CR7 Hotel ipo katika eneo la Madeira ambapo ndipo mchezaji huyo alipokulia. Katika hoteli hiyo kuna baaadhi ya maeneo yenye picha za Ronaldo, Makombe, tuzo zake na sehemu nyingine ni muonekano wa nyasi za uwanjani.

Licha ya muonekano wake kuwa wa hadhi ya juu sana, gharama za kulala hapo usiku mmoja ni £184 (TZS 527,166.5). Aidha taarifa zinaeleza kuwa mchezaji huyo anampango wa kujenga hoteli kama hiyo katika miji ya Lisbon, Madrid, and New York City.

Cristiano Ronaldo ndiye mchezaji anayevuta mkwanja mrefu zaidi Duniani,

 

Wadau Wa Michezo Watakiwa Kushirikiana Na Serikali Kuinua Michezo
Mgogoro wa Kota za Magomeni Umekwisha