Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema kuwa Muungano ni kitu muhimu ambacho kinaleta mshikamano katika kuleta maendeleo ya nchi.

Ameyasema hayo Ofisini kwake jijini Dar Es salaam na kuelezea maana harithi ya muungano, ambapo amesema kuwa muungano huo ni muhimu kwa mustakabari wa nchi.

Amesema kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni mfano wa kuigwa kwani hakuna muungano kama huo uliodumu kwa muda mrefu zaidi duniani.

“Huu Muungano wa kihistoria duniani, tuko huru katika muungano huu, huwezi kulinganisha na nchi zingine duniani, na nitoe rai kwa wananchi tuwajenge watoto wetu katika uzalendo,”amesema Polepole

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Aprili 27, 2018
Niyonzima: Tukiifunga Young Africans shughuli imekwisha

Comments

comments