Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amemtaka Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo kuacha kuuhadaa umma.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kiongozi huyo amekuwa akijenga hoja za uongo.

Aidha, Polepole ameipongeza serikali ya Chama cha Mapinduzi kwa kuweka hadharani ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali na kuanza kuwachukulia hatua wale wote waliohusika katika ubadhilifu.

“Huyu Zitto Kabwe amekuwa akijenga hoja nyingi za uongo kwa lengo la kupotosha umma, kila jambo zuri linalofanywa na serikali analififisha, hii tabia ni ya hovyo,”amesema Polepole

Mwizi wa fedha kwa njia ya mtandao anusurika kifo
Rais JPM afanya uteuzi wa nafasi 9

Comments

comments