Chama Cha Mapinduzi kimeitaka Serikali kuchukua hatua za haraka kuhusu matukio ya Mauaji yanayoendelea katika wilaya za Kibiti, Mkuranga na Rufiji Mkoani Pwani ili kuepusha mauaji hayo kuendelea kutokea.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole, mapema hii Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mauaji yanayoendelea katika Wilaya hizo.

Polepole amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha vinaelekeza akili, nguvu zao katika Wilaya hizo kwa kuwa mauajia hayo yanasababisha kuzorota kwa shughuli za maendeleo.

Aidha, ameongeza kuwa kwa muda mrefu sasa chama kimekaa kimya kikiamini hatua zitachukuliwa kwa kuwa wanachama wake na watendaji wameendelea kupoteza maisha ambapo amesema kwa sasa inatosha.

Hata hivyo, Kuhusu suala la uchaguzi ambao unaendelea ndani ya Chama hicho amesema mauaji hayo yanakiweka Chama katika mazingira magumu ya kufanya chaguzi zake hivyo ni vema hatua zikachukuliwa sasa.

Njiwa anaswa akisafirisha dawa za kulevya
Singida United yazidi kufanya kufuru katika usajili