Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema kuwa kuna wabunge wengine watatu kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jijini Dar es salaam wameomba kujiunga na CCM.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa kuna idadi kubwa ya viongozi kutoka vyama vya upinzani hasa Chadema wameomba kujiunga na CCM.

Amesema kuwa kwasasa kuna wimbi kubwa la viongozi ambao wamekuwa wakijiuzulu vyama vya upinzani na kujitangaza kuwa wamehamia CCM.

“Kwakweli kwasasa tunafanyakazi ya kuwazuia baadhi ya viongozi wa upinzani kujiunga na chama chetu, tunachambua kwanza CV zao ndio tunawaruhusu, na niwahakikishie tu kwamba hakuna anayenunuliwa hata mmoja, wanakuja kwa kuvutiwa na kazi nzuri inayofanywa na Rais Magufuli,”amesema Polepole

Rais Magufuli afanya uteuzi mwingine wizara ya mambo ya nje
Lil Wayne atangaza tarehe ya kuachia 'Tha Carter V'