Jeshi la Polisi nchini Marekani limesema kuwa halitamfungulia mashtaka ya aina yoyote mwanaume mwenye asili ya ‘kizungu’ aliyempiga risasi na kumuua ‘kijana mweusi’ wakati wa mabishano.

Tukio hilo la mauaji lilitokea wiki iliyopita katika eneo la Clearwater, Florida.

Michael Drejka mwenye umri wa miaka 47 alimfyatulia risasi Markeis McGlockton na kusababisha kifo chake, baada ya kijana huyo kumsukuma kwa nguvu hadi kuanguka chini kufuatia ugomvi uliozuka wakati wakibishana kuhusu eneo la kuegesha magari.

Video ya tukio hilo iliyozua gumzo kwenye vyombo vya habari inamuonesha Markeis McGlockton akimsukuma vibaya Drejka na kumuangusha chini huku rafiki yake akiwa anaangalia. Hata hivyo, Drejka aliamua kujitetea kwa nguvu kubwa akiwa bado yuko chini akitoa bastola na kumfyatulia risasi kijana huyo ambaye alikufa alipokuwa katika hatua za matibabu hospitalini.

Drejka amefanikiwa kukwepa kufunguliwa mashtaka kufuatia sheria ya kujilinda inayozua utata nchini humo. Tukio hilo limeibua hisia kali kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya mkondo mkuu likihusishwa na ubaguzi wa rangi kutokana na maamuzi ya jeshi la polisi.

Mwanamke ambaye ni mpenzi wa McGlockton aliyekuwa anashuhudia tukio hilo akiwa kwenye gari, alisema kuwa mfyatua risasi alizua tafrani na alikuwa na lengo la kuamsha hasira za mtu.

Mkuu wa polisi wa eneo hilo, Gualtieri aliwaambia waandishi wa habari kuwa hatamfungulia mashtaka Drejka kwa sababu anaamini kitendo chake kinalindwa na sheria ya Florida inayojulikana kama ‘Stand your ground’.

Sheria hiyo inamruhusu mtu kutumia nguvu hata kuua pale anapoamini yuko kwenye hatari ya kuuawa.

Video: Chadema wajilipua, Polisi waliohusishwa mauaji ya Akwilina huru
Mayweather awalipa mashabiki mamilioni kumtukana 50 Cent

Comments

comments