Msemaji wa jeshi la polisi Tanzania, Kamishna msaidizi  polisi Barnabas Mwakalukwa amesema hakuna mbwa wa polisi aliyepotea katika kikosi cha mbwa na farasi kama ambavyo iliripotiwa siku chache zilizopita.

Leo Mwakalukwa amezungumza na vyombo vya habari alipotembelea kikosi hiko Jijini Dar es salaam ambapo amesema wakati wa ziara ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola bandarini mbwa huyo alikuwa katika mafunzo maalumu yaliyokuwa yakifanyika katika bwalo la polisi Osterbay yaliyoanza Julai 10 na kutarajiwa kumalizika Septemba 21 mwaka huu.

Hata hivyo amesema kwamba mbwa aliyepotea anaitwa Gilo na si Hobby kama ambavyo ilikuwa inajulikana hapo awali.

Hivyo ameomba watanzania waendelee kuliamini jeshi la polisi kwa kazi ya ulinzi wanayoifanya.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Agosti 2, 2018
Video: Polisi wafunguka kuhusu kumkamata Zitto Kabwe, "Tunafanya kazi kwa weledi"