Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es salaam, (UDSM) Prof. Benson Bana amepongeza kitendo cha rais Uhuru Kenyatta kukutana na mpinzani wake mkuu kutoka NASA, Raila Odinga kumaliza tofauti zao.

Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa matatizo ya Waafrika yatamalizwa na Waafrika.

Amesema kuwa kitendo hicho cha kukutana kwa mahasimu hao wa kisiasa kinapaswa kuigwa na wanasiasa wa nchi zingine za Kiafrika.

“Sisi tunaliona jambo hilo ni la kuigwa na ni jambo jema ambalo nchi nyingine za Kiafrika zinapaswa kujifunza, tunapokuwa na tofauti zetu za ndani, viongozi wa kisiasa wanapaswa kumalizana,”amesema Prof. Bana

 

Magazeti ya Tanzania leo Machi 14, 2018
UN yawapa tano Uhuru Kenyatta na Raila Odinga

Comments

comments