Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es salaam (UDSM), Prof. Benson Bana amewataka wanasiasa kutumia lugha yenye staha pindi wanapoikosoa serikali.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa sio lazima kutumia lugha zenye ukakasi wakati wa kuikosoa Serikali.

Amesema kuwa wanasiasa wengi wamekuwa wakitumia lugha chafu dhidi ya rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kitu ambacho amesema sio sahihi.

“Kusimama kwenye majukwaa na kutoa maneno yasiyokuwa na staha siyo kitu kizuri, wanatakiwa kuheshimu mamlaka iliyowekwa na Watanzania,”amesema Prof. Bana

 

 

Magazeti ya Tanzania leo Machi 15, 2018
Harmonize awatoa machozi mashabiki wake....'Jifunze kutokata tamaa'