Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Prof. Ibrahim Lipumba amelalamikia kufanyika hujuma dhidi ya wagombea wake waliojitokeza kuwania nafasi za Udiwani katika baadhi ya Kata ambazo zina uchaguzi wa marudio.

Ameyasema hayo Jijini Dar es salaam wakati akifungua mkutano wa baraza kuu la chama hicho, ambapo amesema kuwa wagombea wa chama hicho katika kata ya Luwaruke, Kisiju, pamoja na kata ya njia nne wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani wameshindwa kurudisha fomu za udiwani kwa viongozi wa kata.

“Kulivyotangazwa Uchaguzi tukasema tutaweka wagombea lakini wengine jana wakati wanarejesha fomu walikamatwa kwa madai ya kughushi muhuli, na nikitoka hapa mimi na wagombea tutaelekea tume kufikisha madai yetu, ili wasiseme mambo haya yameishia kwenye vyombo vya habari, tukihitaji demokrasia lazima tufuate taratibu” amesema Prof. Lipumba.

Hata hivyo, Prof. Lipumba amekosoa kitendo cha baadhi ya viongozi wa upinzani kutangaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa madai ya kuunga mkono juhudi za chama hicho na kusema hawana sababu za msingi.

 

Kangi Lugola atoa angalizo kuhusu ajali ya MV Nyerere
Breaking News: Waziri Lugola akizungumza eneo la tukio ajali ya MV Nyerere