Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Prof. Ibrahim Lipumba amesema kuwa viongozi wa kisiasa, Edward Lowassa (CCM) na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, wanasumbuliwa na tamaa ya madaraka.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo ameelezea sakata zima la Edward Lowassa kurudi Chama chake cha zamani, CCM, anasumbuliwa na tamaa ya madaraka.

Amesema kuwa tangu ahamie upinzani hakuna kilichofanyika hivyo, maaamuzi ya kurudi kwake kwenye chama chake cha zamani ni sahihi.

Katika hatua nyingine Prof. Lipumba amemshangaa Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad na kusema kuwa wapinzani walifanya makosa kwakuwa siku zote walikuwa wanasimamia sera zao.

”Nawashangaa sana hawa wapinzani wenzangu kwa kumpokea kipindi kile na kumfanya Dkt. Slaa kuondoka, sasa wamejionea wenyewe kile walichokitaka, na hili ni funzo,”amesema Prof. Lipumba

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Machi 7, 2019
Real Madrid yamnyapia Mbappe ikimtema Bale