Mwenyekiti wa kamati ya uongozi ya chama cha wananchi( CUF ), Julius Mtatiro amesema kilichotekwa na Prof.  Lipumba ni majengo ya ofisi za chama hicho na wala si chama, amesema shughuli za chama hicho zinaendelea kama kawaida kwani yeye ndiye Mwenyekiti wa CUF na siyo Prof. Lipumba aliyedai kuwa amewekwa katika ofisi za CUF na Chama cha Mapinduzi (CCM) , Msajiri wa Vyama vya Siasa na Jeshi la Polisi.

Mtatiro amesema chama cha kiasa ni vikao vya chama, wanachama na shughuli za chama, kwahiyo vyote hivyo vinaendelea ndani ya CUF hata nje ya ofisi na Prof. Lipumba hajasimamisha shughuli yoyote ya chama hicho. Bofya hapa kutazama video

Francesco Guidolin "Out", Bob Bradley "In"
Wizara ya ardhi ya adhimisha siku ya makazi Duniani