Quick Rocka ameachia rasmi video ya wimbo alioubatiza jina la ‘Down’ akimpa shavu Mimi Mars ambaye ni mdogo wake Vanessa Mdee. Hii imekuwa kolabo ya kwanza kubwa kwa Mimi Mars, tangu atambulishwe rasmi kwenye muziki.

‘Down’ ni wimbo wa shangwe za ‘club’ wenye ujumbe wa mapenzi kutoka kwa jamaa aliyedata na mrembo wake na anamshawishi mrembo huyo aoneshe ‘maufundi’ ya kuchezesha mwili wake kufuata mdundo unaokita kwenye spika za eneo la starehe, kwa ajili yake.

“Down is a party love song (… ni wimbo wa shangwe na mapenzi),” Quick Rocka anaeleza maana ya jumla ya wimbo wake.

Video ya wimbo huo ambao audio yake imepikwa ndani ya Switch Records, imeongozwa na Hanscana.

Quick ambaye alitambulishwa kwenye ulimwengu wa muziki kupitia wimbo wa ‘Bullet’ ambao uligeuka kuwa ‘Wimbo wa Taifa’ miaka takribani saba iliyopita akiwa mkali wa kurap kwa mwendo kasi mithiri ya treni ya umeme, ameshusha sauti na mwendo kwenye Down kumshawishi mrembo wake.

Magazeti ya Tanzania leo Aprili 22, 2017
Video: Diamond azindua 'Chibu Perfume', atoa neno kwa wasanii nchini