Mkurugenzi Mkuu wa CZ Information & Media Consultant LTD, Cyprian Majura Nyamagambile amesema kuwa Rais hataki kuongoza miaka saba lakini wao wanataka kwakuwa wana haki ya kutoa maoni yao kama wananchi.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amelitaka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanya mabadiliko ya vipengele vya Katiba ili iweze kumuwezesha rais kutawala kwa muda wa miaka saba.

“Rais Dkt. Magufuli alishasema hataki miaka saba. hata juzi karudia tena kwamba hataki lakini sisi tunataka miaka saba, na tunaliomba bunge libadili Katiba,”amesema Nyamagambile

Hata hivyo, ameongeza kuwa Rais Magufuli ni wa mfano wa kuigwa Afrika kwa yale anayoyafanya kwani wengi wameshindwa lakini yeye ameweza.

Wanne wapelekwa kamati ya maadili TFF
Utajiri wa Kakobe wageuka mbele ya TRA, ‘namwaga mboga’