Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amewatakia Waislamu wote Mfungo mwema wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani pia Rais amewataka wafanyabiashara kutopandisha bei za vyakula hususani vile vinavyotumika zaidi wakati huu wa Ramadhani.

“Kwa niaba ya serikali na mimi mwenyewe na Watanzania kwa ujumla, napenda kutumia fursa hii adhimu kuwatakia Waislamu wote nchini Tanzania mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, uwe mfungo wa amani na wenye baraka, lakini pia ninamuomba Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema azikubali funga zenu na kuwalipa malipo stahiki” – Rais Magufuli

Rais Magufuli pia aliwahakikishia Watanzania wote kuwa serikali yake ipo imara kuhakikisha inalinda na kuidumisha amani iliyopo.

Tite Arithishwa Mikoba Ya Carlos Dunga
Aomba Radhi Kwa Kitendo Cha Kunusa Sehemu Za Siri