Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amempatia kiasi cha shilingi 200,000, Rashid Mashaushi mkazi wa Kinondoni mara baada ya kutoa kero za mtaani kwake.

Akizungumza mbele ya rais, Mashaushi amelalamikia barabara ya mtaani kwake kuwa ni mbovu na imekuwa ikisababisha mafuriko kipindi cha masika.

Aidha, katika hatua nyingine rais Dkt. Magufuli amemuagiza mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kuhakikisha barabara hiyo inajengwa kwa gharama.

“Mkuu wa mkoa chukua namba yake, utampigia akupeleke katika eneo husika ili uweze kulishughulikia suala la ujenzi wa barabara hiyo,”amesema rais Dkt. Magufuli

Hata hivyo, rais Magufuli leo alifanya ziara ya ukaguzi wa ofisi za Baraza la Waislam Tanzania (BAKWATA)

 

Ukifanya haya 7 kila siku utajikinga na magonjwa ya moyo
Makonda atumia mamilioni kuwakatia Bima ya Afya watoto yatima

Comments

comments