Rais Mstaafu wa Awamu ya pili wa Tanzania,  Alhaj Ali Hassan Mwinyi amempongeza Rais wa awamu ya tano, Dk. John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya na yenye mafanikio makubwa kwa Taifa.

Mwingi amesema hayo leo Novemba 23, 2016 wakati alipomtembelea Rais Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam ambapo amesema amemtembelea Rais Magufuli ili kumpongeza kwa kazi nzuri sana anayoifanya tena kwa muda mfupi, amesema kwa kazi zake nzuri anahitaji msaada wa kumuombea dua na kurekebisha kusema kweli pale watu wanapopotosha.

Akizungumzia ruswa amesema kuwa Rais Magufuli ameonyesha uimara mkubwa tofauti na viongozi wengine kwani rushwa ilikuwepo tangu enzi ya Hayati Mwalimu Nyerere, aliipondaponda kabisa lakini hakuimaliza, na wengine waliofuatia walifanya hivyo hivyo, kila mmoja amefanya kwa kiasi chake, lakini Rais Magufuli kwa mwaka mmoja ameleta Sunami, nafurahi sana. Tazama hapa

Diamond awachana ‘Team Kiba’, adai wanakimbia akiwaomba pambano
Mzee Mwinyi akiri Magufuli ‘amefunika’ kazi ya watangulizi wake