Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza mchakato wa msamaha wa kodi kwa vifaa vya mradi wa ujenzi wa meli mpya, ukarabati wa meli za Mv Victoria na Mv Butiama ukamilike haraka.

Ametoa agizo hilo jijini Mwanza wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo la ujenzi na ukarabati wa meli mpya ambapo amewataka makatibu wakuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na katibu mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango kuharakisha mchakato huo.

Akizungumza kwa njia ya simu akiwa ziarani mkoani Mwanza akikagua ujenzi huo katika eneo la Mwanza Kusini, Rais Magufuli amewaagiza watendaji hao kukaa pamoja kumaliza taratibu zinazotakiwa ili vifaa hivyo vifike Mwanza.

Aidha, ametoa agizo hilo mara baada ya kuambiwa kuna makontena ya vifaa vya ujenzi wa meli hizo bandarini na hivyo kukwamisha ujenzi wa meli hizo.

Kabla ya kutoa maagizo hayo, Rais Magufuli alimuuliza msimamizi wa Meli hizo kuhusu maendeleo ya ujenzi huo, na kumtaka ampigie simu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano kuhoji vifaa hivyo.

Balozi Seif Idd atembelea eneo zitakapojengwa ofisi za SMZ
Bulembo atoa msaada katika kituo cha afya Zamuzamu