Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli atazindua rasmi mradi wa mabasi ya mwendokasi jijini Dar es salaam.

Akitoa taarifa hiyo, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewataka wananchi kujitokeza kesho muda wa saa mbili asubuhi katika eneo la Gerezani, Kariakoo kushuhudia uzinduzi huo uliopata kibali kutoka kwa Rais kuanza kwa majaribio tangu mwaka jana. amesema mradi huo ni miongoni mwa miradi ya kujivunia kwani umekuwa msaada mkubwa sana kwa wananchi wa Dar es salaam ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais Magufuli.

AFCON 2017: Congo DRC Mwendo Mdundo
Fahamu nchi zinazolipa mishahara ya kima cha chini