Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Ally Hapi, amesema kuwa Tanzania inatarajia kupata ugeni wa Rais wa Jamhuri ya Uturuki Tayyid Erdogan ambaye anatarajiwa kuwasili nchini  tarehe 22/01/2017 katika uwanja wa J.K Nyerere na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, Hapi amesema ziara ya Rais huyo wa Uturuki nchini ni ya kiserikali ambayo itakuwa siku mbili kwa mwaliko wa mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rais wa Uturuki atapokelewa  siku ya Jumatatu Ikulu na mwenyeji wake na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, kisha kusaini mikataba mbalimbali ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili.

Aidha,Rais huyo anatarajia kukutana na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Mohamed Shein kwa mazungumzo mafupi,pia kufanya mazungumzo na wafanyabiashara katika Hotel ya Hyatt Regency.

Hata hivyo, Hapi amesema Rais huyo ataambatana na ujumbe mkubwa wa watu tisini, wakiwemo viongozi

Jammeh akubali kuachia madaraka
Video: Baraza la ujenzi la Taifa lafanya ukaguzi wa miradi ya ujenzi