Leo Oktoba 7, 2016 Rais wa Colombia, Juan Manuel Santos ametangazwa kuwa mshindi wa  Tuzo ya Amani ya Nobel 2016 licha ya kuvunjika kwa mkataba wake wa kusitisha vita na waasi wa Farc nchini humo.

Rais Santos alifanikiwa kufikia makubaliano ya amani na waasi wa Farc jambo ambalo lilifikisha kikomo vita vilivyodumu kwa karibu miaka hamsini.

Makubaliano hayo yalitiwa saini na Rais Santos na kiongozi wa waasi hao Rodrigo Londono, maarufa kwa jina la Timochenko mjini Cartagena tarehe 27 Septemba.

Waasi wa Farc, ambao walianza kama wanamgambo wa Chama cha Kikomunisti mwaka 1964, wanatarajiwa kuacha vita na kuingia katika siasa za amani.

Kiba: Huwezi kumuoa mtu kama hamuelewami.
Tandale walaumu jeshi la polisi