Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewatangazia wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na Tanzania kwa jumla kuhusu ujio wa Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda na Rais Danny Faure wa Shelisheli.

Makonda amesema wageni hao wanatarajiwa kufika nchini kwa ziara ya siku mbili, ambapo Rais wa Uganda, Yoweri Museveni atawasili kuanzia Februari 25 hadi Februari 26, 2017 na Rais wa Shelisheli, Danny Faure akitarajiwa kuwasili Februari 27 hadi Februari 28, 2017.

Amesema kuwa ujio wa marais hao unazidi kudhihirisha kuwa Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli inaheshimika na kuthaminiwa katika siasa za kimataifa

Mawaziri 15 wa Nchi za SADC kukutana Dar kesho
Adam Lallana: Liverpool Ni Mahala Sahihi Kwangu