Hali ya mwimbaji Ray C sio nzuri, ana hinahitaji msaada wa haraka kwani hivi sasa ameanza kuingia mikononi mwa vyombo vya dola kutokana na matumizi ya dawa za kulevya.

Mwimbaji huyo ambaye awali alisaidiwa kutoka kwenye matumizi ya dawa hizo na Rais mstaafu, Jakaya Kikwete na kurudia kwa kiasi kikubwa hali yake, ameonekana kwenye kipande cha video akitiwa mbaroni na kupandishwa kwenye gari la Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam.

Katika video hiyo, Ray C ambaye amekamatwa na wenzake anaonesha kutowatambua askari hao akidhani ni wahuni waliomteka hivyo anaomba msaada.


Hivi karibuni, Ray C aliweka wazi kuzidiwa nguvu na dawa za kulevya akieleza kuwa amekuwa akishindwa kupata dawa za kumsaidia kuondokana na uteja na kwamba hali yake ya kifedha imekuwa ngumu kupitiliza hadi nauli ya basi kwenda hosptali kupata dawa hizo imekuwa ngumu.

Video: Gwajima awindwa. Majanga matano uzimaji wa simu feki. Mkapa jipu kuu - Magazeti leo
Ulimi wamponza tena Gwajima, Polisi wamuwinda