Msanii na mtunzi wa mashairi ya muziki wa Bongo fleva nchini anayefanya kazi chini ya lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Rayvany baada ya kutangaza kwa siku kadhaa ujio wa ngoma yake mpya inayoenda kwa jina la ”Pochi nene” kupitia mitandao yake ya kijamii, tayari ngoma hiyo imeachiwa rasmi.

Wimbo huo amemshirikisha msanii S2Kizzy, ngoma hiyo inaendelea kufanya vizuri katika chati za video zinaoongoza kutazamwa zaidi katika mtandao wa You Tube.

Aidha hivi karibuni msanii Harmonize naye ameachia ngoma yake inayoenda kwa jina la Dm Chick aliyofanya na msanii maarufu toka Ghana, sasa ni zamu ya Rayvany

Kutazama wimbo huo bonyeza kitufe chekundu hapo chini, kisha mpe alama zako msanii huyu kwa kazi hii mpya.

Video: Mbunge Chadema ampigia magoti Rais Dkt. Magufuli
Video: Magufuli azindua daraja jipya lililopewa jina lake