Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewataka wabunge wanaotoka katika mkoa anaouongoza kufanya ziara kusikiliza kero za wananchi ili waweze kuzitatua.

Amesema kuwa wabunge wengi wamekuwa wakisubiri uchaguzi ndipo waanze ziara za kuwatembelea wananchi, lakini amewatadharisha wanaotoka katika mkoa wake kwamba wasijisumbue kufanya hivyo kwani 2020 wataisikia tu.

Ameyasema hayo wilayani Kigamboni jijini Dar esalaam, wakati wa uzinduzi wa ofisi za walimu Shule ya Msingi Vijibweni zilizojengwa kwa ufadhili wa kampuni ya CRJE (East Africa) Limited ya China.

“Mimi nahangaika kujenga majengo na wao basi wahangaike kuleta madawati, lakini kama wakisubiri mpaka ukaribie uchaguzi wa 2020, kama nitaendelea kuwepo, hii itakuwa imekula kwao, wahesabu maumivu,”amesema RC Makonda

Aidha, katika hatua nyingine, Makonda amesema kuwa alikula kiapo mbele ya Rais na Mwenyezi Mungu, hivyo hatatumia nafasi yake kwa manufaa binafsi bali kwa wananchi aliopewa kuwaongoza.

Hata hivyo, Makonda ameongeza kuwa hakuna kitu kinachouma kama dhamira yako ni ya kweli harafu mtu anakurudisha nyuma, huku akiongeza kuwa wao serikalini wana uwajibikaji wa pamoja.

Wapinzani watangaza maandamano nchini Sudan
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 9, 2019