Msanii kutoka lebo ya WCB, Rich Mavoko ametoa video mpya inayoenda kwa jina la Sheri akiwa amemshirikisha msanii wa muziki wa  hip pop Fid Q.

Kutoka lebo ya Wasafi, msanii Diamonnd tayari akiwa ameshaachia ngoma zake zakutosha, sasa imefika zamu ya rich mavoko nae kufanya yake na ameachia ngoma kali sana inaitwa Sheri.

Moja ya ‘interview’ Mavoko alihojiwa kuhusu menejimenti ya kundi la wasafi kumpendelea Diamond Platinumz zaidi kikazi kuliko msanii mwingine yeyote, Mavoko alikanusha kauli hiyo na kuitetea menejimenti kuwa inafanya kazi bila upendeleo wowote.

Lakini hayo yanaweza kudhihirishwa kwa kuangalia listi ya nyimbo zilizofanywa na msanii mmoja mmoja  katika kundi la Wasafi na mpaka sasa Diamond Platinumz anaoongoza kufululiza kuachia kazi zake kama Eneka, Mary You, I miss you, Fire na Rokonolo,  kuliko msanii mwingine yeyote toka lebo ya WCB.

Tazama video hapo chini ya Sheri hapa chini.

Gambo awanyooshea kidole wanaoingiza siasa kwenye masuala ya maendeleo
Werema afunguka kwanini alimuita Kafulila ‘Tumbili’