Rihanna amekuwa mmoja kati ya nyota watakaoing’arisha filamu mpya ya Ocean’s 8, itakayoingia kwenye kumbi za sinema kuanzia Juni 8 mwaka huu.

Katika kionjo cha filamu hiyo kilichoachiwa hivi karibuni, RiRi ameonekana akiwa katikati ya mchakato wa kuiba almasi ya mabilioni ya fedha na kundi la warembo.

Rihanna anatumika kama mtaalam wa computer ambaye anafanya udukuzi kwenye mifumo ya wenye pesa na mali.

Debbie Ocean (Bullock) na timu yake ya wataalam akiwemo Rihanna wanapanga kufanya wizi/ujambazi mkubwa. Wamelenga kuiba $150 milioni ambayo ni thamani ya almasi kutoka kwa muigizaji maarufu, Daphne Kluger (Hathaway).

Filamu hiyo iliyoongozwa na Gary Ross inachombezwa na wimbo wa miaka ya 1970 ‘You’re No Good’ wa Linda Ronstadt.

Waigizaji wengine ni Sandra Bullock, Cate Blanchett, Anne Hathaway, Mindy Kaling, Sarah Paulson, Awkwafina na Helena Bonham Carter.

Rihanna ameendelea kung’aa kwenye muziki lakini haiachii fursa yoyote ya kipaji anachoweza kukitumia kuingiza fedha nyingi.

Hifadhi vizuri kumbukumbu ya Juni 8 mwaka huu, wiki chache baada ya kuzinduliwa Marekani, utaweza kuiona hapa nchini ‘Ocean’s 8’.
Angalia kionjo hapa:

UEFA Europa League nusu fainali yaanikwa hadharani
Boko Haram wateka wasichana 1000

Comments

comments