Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Rin Marii ambaye wiki kadhaa zilizopita alifungua pazia la Bongo Flava kwa kishindo cha video ya wimbo wake wa ‘Salaam’, amefunguka kuhusu tuhuma za Diamond Platnumz kwa wasanii wa kike kuwa wana wapenzi wengi hali inayomfanya asimruhusu mtoto wake Tiffah kuwa msanii.

Kupitia mahojiano rasmi aliyofanya na Dar24, Rin Marii ametoa ushauri kwa Diamond, pia ameeleza sababu zilizopelekea yeye kuingia kwenye muziki na kufanya kazi yake ya kwanza iliyovuta sikio la ‘Wanene Entertainment’, waliokubali kupika audio na video ya ‘Salaam’.

Msanii huyo wa kike ambaye uwezo wake mkubwa unatoa picha ya njia nzuri ya kuelekea kwenye kilele cha mafanikio ya muziki wa mkondo mkuu, amesema kuwa ameanza kujihusisha rasmi na muziki wakati huu akiwa mfanyakazi wa kampuni moja jijini Dar es Salaam kutokana na kuufanyia kazi ushauri wa kutakiwa kusubiri hadi amalize shule.

Katika hatua nyingine, Dar24 ilimuomba Rin kueleza kile ambacho angemwambia ‘Simba’, Diamond Platinumz kuhusu mwanae wa kike, Tiffah kufuatia kauli yake kuwa asingependa mwanae huyo awe mwanamuziki siku za usoni akihofia kuwa wanaume watamrubuni sana.

Mkali huyo pia ameeleza jinsi alivyorekodi na kushuti video yake, uhusiano wake na kijana mtanashati anayeonekana kwenye video yake, mpango wake katika safari aliyoianzisha na mengine mengi. Usikose kuangalia video iliyoambatishwa kwnye habari hii uyapate yote kiundani.

Video: Taarifa ya TFDA kuhusu mchele wa plastiki
Wydad Casablanca Kuamua Hatma Ya Al Ahly

Comments

comments