Muimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania, Rose Muhando ametoa shukrani kwa Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na wananchi wake kwa kumsaidia kipindi alipokuwa na matatizo ya afya.

Ambapo mwaka jana kulisambaa baadhi ya video zikimuonesha akiwa katika moja ya kanisa akifanyiwa maombi ya kutolewa mapepo Jijini Nairobi kwa kudaiwa kutumia madawa ya kulevya yaliyomdhoofisha.

Shukrani hizo amezitoa kupitia wimbo wake mpya aliouachia Jumanne, Septemba 24 akiwashukuru juu ya uponyaji uliofanyika pindi akiwa katika ardhi hiyo ya Kenya.

“Shukrani zangu kwa taifa viongozi na wananchi wa Kenya kwa kuokoa maisha yangu, mlifungua milango yenu na kunikaribisha kwa mikono yenu miwili. Kwa hakika Kenya ilinionesha neema. Sijui jinsi ambavyo ninaweza kuwalipa kwa upendo wenu kwa kuwa mimi si tajiri lakini naomba Mungu aibariki Kenya”, ni sehemu ya maneno yaliyopo katika wimbo huo wa Rose Muhando.

Kabla ya skendo hizo Rose Muhando amewahi kuwa moja ya waimbaji injili wakubwa Tanzania ambazo zilimpa umaarufu mkubwa, lakini baadae umaarufu ulipungua na kupotea kabisa hadi pale taarifa zake za matumizi ya madawa ya kulevya kuanza kutapakaa kwenye mitandao ya kijamii na kupelekea Serikali kuingilia kati na kuamuru afanyiwe matibabu.

Daktari awashauri wanaume kulia, 'msihofie kuchekwa'
Serikali yasitisha vibali ujenzi miradi ya Maji