Mtangazaji wa kituo cha habari cha CloudsFm, Fredy Fideris amesema kuwa atamkumbuka kwa vitu vingi Ruge Mutahaba kwani ameweza kumsaidia hata kabla hajaanza kufanya kazi katika kituo hicho cha redio.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media ambapo amesema kuwa yeye na Ruge Mutahaba walifahamiana zamani, hivyo alimuongoza kwa vitu vingi katika kuhakikisha anafanikiwa katika maisha.

”Kwakweli Ruge Mutahaba kwangu mimi alikuwa kama kaka mwenye akili kubwa sana, nilikuwa nikimsikiliza kwa vitu vingi, nimeshafanya mahojiano naye mara nyingi sana, alikuwa anapenda sana vijana tufanikiwe,”amesema Fredy

Mamilioni yamwagwa kwa Walimu wastaafu Njombe
Video: Majaliwa atoa neno kwenye msiba wa Ruge

Comments

comments