Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group (CMG), Ruge Mutahaba amesema kuwa kwa sasa hawana tatizo lolote na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam mara baada ya kupatanishwa na Rais Dkt. John Magufuli.

Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam kwenye mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), ambapo amesema kuwa tofauti iliyokuwepo ilimalizika tangu jumamos iliyopita hivyo kwa leo hapakuwa na haja ya kuongelea suala hilo.

“Kwanza niseme tu kwamba sikutarajia kuwa ninakuja tena kuongelea suala ambalo tayari lilishamalizwa na Rais Dkt. Magufuli, lakini kwa sababu wameniita basi ngoja tulimalize tena na Jukwaa la Wahariri, ila tu ikumbukwe kwamba suala hili limeshamalizika,”amesema Ruge

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema kuwa alikuwa akiwasiliana mara kwa mara na Jukwaa hilo ili waweze kuangalia namna ya kumaliza tatizo hilo ili mambo mengine yasonge mbele.

Naye Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Theofili Makunga amesema kuwa Jukwaa limefanya kila jitihada za kuweza kutatua mgogoro huo uliojitokeza baina ya mkuu huyo wa  mkoa na chombo hicho cha habari.

Edu boy atoa fursa kwa wasanii wa nyumbani 
Serikali yatoa onyo dhidi ya wananchi wanaouza ardhi