Machi 21, 1955 Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliporudi shuleni Pugu (shule aliyokuwa akifundisha) akitokea Umoja wa Mataifa nchini Marekani, alitakiwa achague kuacha ualimu au siasa.

Mwalimu Nyerere aliamua kuacha ualimu ili aendelee kuongoza harakati za kutafuta uhuru, huku akiwa hana hakika siasa ingemfikisha wapi.

Hivyo aliacha kazi iliyokuwa ikimpatia riziki kwa ajili ya Taifa lake. Huo haukuwa uzalendo wa kawaida.

Aliendelea na juhudi za kutafuta uhuru bila kukata tamaa kwani alikuwa jasiri, angekuwa mtu wa kukata tamaa basi asingechelewa kuondokana na uongozi wa TANU (alikuwa Rais wa TANU).

Mkutano wa kwanza wa TANU uliohutubiwa na Mwalimu Nyerere mjini Masasi mwaka 1955 ulihudhuriwa na watu kumi na mmoja tu.

Pamoja na hali ya kukatisha tamaa lakini Mwalimu Nyerere alikusudia kutimiza kusudio la kupatikana kwa uhuru Tanganyika, kwani lengo la kwanza la TANU lilikuwa kuleta Uhuru wa Tanganyika na kazi ya kwanza ya TANU ilikuwa kuwatayarisha Watanganyika kwa kujitawala wenyewe.

Kutokana na harakati za kutafuta uhuru wa Tanganyika zilizoongozwa na Mwalimu Nyerere kutokuwa rahisi, baada ya kupatikana kwa uhuru, Nyerere aliitwa “Baba wa Taifa” ikiwa na maana ya mtu aliyeongoza juhudi za kutafuta uhuru na ujenzi wa Taifa jipya.

Tamasha la Fiesta latangazwa upya, litafanyika hapa
LIVE: Rais Magufuli na Waziri Mkuu Misri wakishuhudia utiaji saini ujenzi wa mradi wa umeme Rufiji