Homa ya Dengue maarufu kama homa ya kuvunja mifupa ni homa iliyokamata maeneo mbalimbali ya mji wa Dar es salaam, ikiwemo Masaki na Tandale hivyo ni vizuri watanzania kufahamu undani wa ugonjwa huu.

Ni homa ya kuvunja mifupa kwa sababu inamfanya mgonjwa kuwa na maumivu makali hadi kuhisi mifupa inavunjika.

Ugonjwa huu hauna chanjo wala tiba ya moja kwa moja, ila kwenye kipindi cha Afya Tips, Daktari wa magonjwa ya binadamu, Emmanuel Mwakasumi ametoa sababu ya kwa nini tiba ya ugonjwa wa Dengue ni maji na Pandol.

Lakini pia ameweza kueleza sababu za kwa nini wagonjwa wa Dengue hawashauriwi kutumia dawa za kutuliza maumivu aina ya diclofenac.

Tazama hapa chini.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Mei 24, 2019
Serikali kufanya marekebisho ya tozo kwa Wafanyabiashara

Comments

comments