Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar, Salum Mwalimu amefanikiwa kurudisha fomu ya kugombea Ubunge jimbo la Kinondoni huku akiwataka wanachama wa chama hicho kuwa wavumilivu katika kipindi hiki cha muda mfupi.

Ameyasema hayo hii leo Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kurejesha fomu hiyo katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi Manispaa ya Kinondoni,

Amesema kuwa kwasasa hataongea mengi lakini mambo mengine muhimu atayaongea mpaka pale kampeni zitakapoanza rasimi,

“Kikubwa labda niwaambie hatukuja ku-beep wala hatu-beep kamwe haitakuja kutokea ku-beep katika jimbo la Kinondoni. Tunamaanisha na tunaamini kabisa kama nidhamu ya siasa waliyoikataa, hapa watairudisha na wasipoikubali kuirudisha Kinondoni maana yake ustaarabu katika siasa tunaamini utakuwa umekwishamalizika. Hatutokuwa wa kulia, safarii hii ikibidi tutawasababisha wale waliosababisha sisi tunalialia wao ndio walie,”amesema Salum Mwalimu

Polepole ang'aka kuhusu viongozi CCM
Video: Mtulia arejesha fomu, aahidi kufanya makubwa Kinondoni