Mapema wiki hii mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta aliweka historia kwa kuifungia timu yake ya Genk mabao matatu katika mchezo mmoja (Hat Trick) kwenye mchezo wa kuwania kufunzu michuano ya soka barani ulaya, Europa dhidi ya Brondly kutoka Denimark.

Samatta ambaye ametokea kupendwa na mashabiki wa klabu hiyo na kupelekea mashabiki hao kutengeneza wimbo maalumu kwa ajili yake, amezungumzia nafasi za kufunga alizozipata na kuzitumia katika mchezo huo uliomalizika kwa Genk kuibuka na ushindi wa bao 5-0.

Samatta ameongeza kuwa anaamini ataendeleza wimbi la kufunga mabao pindi atakapo kuwa akifata nafasi.

‘Naamini kwenye uwezo wangu, na ninafanya kazi kwa nguvu kwa ajili ya timu yangu kwahivyo nikipata mabao nikama kitu cha ziada kwangu, kwasababu mara zote nataka kushinda, mara zote nataka kuisaidia timu yangu ipate ushindi’’

Samatta ataiongoza Taifa stars kwenye mchezo wa kuwania kufunzu fainali za mataifa ya Africa (Afcon)2019 dhidi ya Uganda Septemba 8 jijini Kampala.

 

Tanzania kinara kesi za haki za binadamu
Mimi sipiganii CCM wala Chadema, niacheni- Musiba