Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amewataka Wakurugenzi walioteuliwa na Rais kutambua dhamana waliyopewa kuwa viongozi wa halmashauri na kwamba wanakwenda huko kuwa watumishi wa umma na siyo watawala.

Kwa upande wa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wawe makini wasije wakajikuta wanaingia kwenye migogoro ya kifedha dhidi ya watendaji wengine, migogoro ya kikazi na pia migogoro na wananchi wanaoenda kuwaongoza.

 “Mkifika huko ninawasihi mshirikiane na wadau wengine ambao ni wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, kamati za ulinzi na usalama, wakuu wa idara, watumishi wa idara mbalimbali zilizo chini yenu na watendaji wa kata na vijiji”- Majaliwa

Jerry Muro Anawa Mikono, ajiweka kando
Polisi kuwasaka wafanyakazi wenye vyeti feki, ‘tutamnyofoa mmojammoja’