Mrembo Selena Gomez amepata ajali ya kwanza jukwaani tangu aanze ziara yake ya ‘Revival’ akiwa Tulsa, Oklahoma, wikendi hii.

Mwimbaji huyo alijikuta akianguka jukwaani akiwa kwenye harakati za kuwapa burudani ya nguvu mashabiki wake akirukaruka kama ndama mwenye furaha. Ghafla, alijikuta akiweka magoti yote chini kwa muda baada ya kutereza lakini aliamua kutumia usanii kulifunika tukio hilo.

“Anguko la kwanza katika ziara yoote, unaweza kuamini imetokea Tulsa?” Alisema Selena Gomez. “Well, I’ll be damned,” alimaliza huku akiinuliwa na shangwe za mashabiki.

Mtanzania Mwingine Akamatwa kwa Kumtukana Rais Kupitia "WhatsApp"
Wabunge wa Ukawa kususia futari, Kusalimiana na wabunge wa ccm