Waziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali ina dhamira ya dhati ya kuboresha sekta ya kilimo ili itoe  mchango unaotegemewa katika ukuaji wa uchumi wa Taifa kupitia sekta ya viwanda.

Majaliwa amesema hayo wakatika kifungua Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, ambapo amekabidhi matrekta 500 kwa wateja wa mwanzo katika awamu ya kwanza ya uunganishaji wa matrekta maalumu kwa ajili ya shughuli za kilimo vijijini.

Amesema kuwa uchumi wa viwanda  ni pamoja  na kilimo, hivyo  ameagiza matrekta hayo yaende vijijini kutekeleza shughuli za kilimo ili kuwaongezea tija wakulima.

Video: Mwigulu Nchemba aibuka, Hii ndio inavyotakiwa
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 5, 2018

Comments

comments