Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema kuwa inategemea kusambaza mifuko maalum vya kujifungulia vyenye vifaa vya kujifungulia kwa wanawake  500,000 ambavyo vitasambazwa nchi nzima kulingana na uhitaji.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Khamis Kigwangalla wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Munira Mustafa Khatibu leo Bungeni Mjini Dodoma.

“Sera ya Afya ya mwaka 2007 inaeleza kuwa Huduma za kina Mama wajawazito katika vituo vya ngazi zote zinapaswa kutolewa bila malipo”, Amesema Kigwangala

Hata hivyo, ameongeza kuwa Serikali haijawahi kuweka tozo na gharama za vifaa vya kujifungulia na upasuaji na hivyo huduma hizo zitaendelea kutolewa katika ngazi zote katika vituo vya umma vya kutolea huduma kwa gharama za Serikali.

Video: Clouds watoe ushahidi - Kamanda Sirro
Video: Waziri Mwigulu atoa onyo kali kuhusu mauaji Kibiti, 'Hatutawaacha...'