Serikali imesema kuwa inatarajia kufunga mitambo mipya ya mionzi ili kuiwezesha hospitali ya Ocean Road kutoa huduma za kibingwa nchini.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Faustine Ndugulile mara baada ya kufanya ziara katika Hospitali ya Ocean Road.

Amesema kuwa serikali ya awamu ya Tano imedhamiria kuhakikisha kuwa huduma zote za kibingwa zinafanyika hapa nchini ili kuweza kuondokana na rufaa za kwenda kutibiwa nje ya nchi.

“Nimefanya ziara katika hospitali hii ya Saratani ya Ocean Road, nimeridhishwa sana na huduma zinazotolewa, hivyo mwezi wa nne tutafunga mitambo ya mionzi,”amesema Dkt. Ndugulile

 

Airtel yazindua duka la huduma za simu jijini Arusha
Shonza afunguka, amtaja Alikiba kuwa mfano wa kuigwa

Comments

comments