Serikali imesema kuwa imetenga Trilioni 1 kwa ajili ya kuwalipa watumishi wa umma na Wakandarasi waliokuwa wakiidai.

Hayo yamesemwa Mjini Dodoma na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema kuwa kwa wafanyakazi wote na Wazabuni wanaoidai serikali wote watalipwa madeni yao mara baada ya uhakiki kukamilika, hivyo watumishi wanatakiwa kuwa wavumilivu.

 

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Machi 6, 2018
Waziri Tizeba mgeni rasmi mchezo wa Simba na Al Masry